Wakati Dunia ikiwa inahangaika na kuzuia maambukizi ya Korona. Timu mbalimbali za Nyumbani zimekuwa zikitumia tatizo hilo kama chanzo kudhoofisha timu za ugenini.

Masuala hayo yameendelea kuonekana yakishamiri sasa baaada ya mechi kati ya Sierra Leone dhidi ya Benin ya kuwania kufuzu AFCON 2022 ambayo ililazimika kuhairishwa baada ya Benin Kudai kwamba Sierra Leone walighushi matokeo ya vipimo vya Korona.

Hii ilipelekea shirikisho la soka barani Africa (CAF) kuhairisha mchezo huo mpaka pale Taarifa nyingine itakapotoka. Katika uwanja wa ndege wa Sierra Leone walipopimwa kugundulika kuwa wachezaji wote walikuwa hawana na maambukizi hayo kama ilivyoelezwa hapo awali.

Mashindano hayo ya kufuzu AFCON 2022 yameshuhudia kesi mbalimbali za timu za ugenini kuonewa. Kenya walieleza kuhusu fitina za aina hiyo hiyo ambapo wachezaji wake wanne muhimu walisingiziwa kuwa na Korona katika mchezo dhidi ya Togo siku ya jumatatu.

Timu ya taifa ya Uganda pia ilishutumu Malawi kufanya vivyo hivyo katika mchezo uliowakutanisha hapo juzi na kushuhudia Malawi wakiibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri. Katika mchezo huu kiungo wao tegemezi Thadeo Lwanga, nyota wa kimataifa wa Simba ya Tanzania alielezwa kuwa na Korona.

UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Korona, Korona Yageuka Sababu Za Kuonea Timu Za Ugenini Afrika, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa