Hakukuwa na mgonjwa wa Virusi vya Corona aliyebainika kutoka katika vipimo 1,195 katika raundi ya hivi karibuni ndani ya Premier league. Uchunguzi wa wachezaji na wafanyakazi wa vilabu ulifanyika mnamo 4 na 5 Juni.

Timu zote 20 zilipitia vipimo maalum vilivyohusisha wachezaji, wahudumu na wafanyakazi wote wa timu husika, hii ni kutokana na kua watu wote wanaoshiriki kukamilisha mchakato wa ligi kuu wanatakiwa kuwa salama na ili kuwakinga wahusika hao, Chama cha soka nchini Uingereza kikishirikiana na Idara ya afya nchini humo kiliandaa utaratibu maalum wa kupima kila mtu ambae atakua karibu na timu hizo.

, Korona Sio Tishio Tena Kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, Meridianbet

Mtu mmoja alikutwa katika duru iliyopita, na jumla kufikia 13 kutoka vipimo 6,274 tangu walipoanza. Premier league iliyosimamishwa tangu Machi 13, imekusudia kuanza bila Mashabiki mnamo 17 Juni wakati Aston Villa itaikaribisha Sheffield United na Mabingwa watetezi, Manchester City kuzuia mitutu ya Arsenal.

Liverpool iko na alama 25 juu ya Msimamo wa PL, wakati Bournemouth, Aston Villa na Norwich City ziko kwenye eneo la kushuka Daraja, Kuna michezo 92 iliyobaki msimu huu kukamilika.

52 MAONI

  1. Mungu aendelee kutupa uzima na afya hili janga lilitupa wakati mgumu na kwa uwezo wake litakwisha kabisa

  2. Bado ni tishio ti ingekuwa sio tishio mashabiki wangeruhusiwa kuingia uwanjani hapo inaonyesha jamaa bado yupooo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa