Toni Kroos alionekana kuongea jmabo na Christiano Ronaldo wakati wa mchezo wa Euro 2020 wa Ureno dhidi ya Ujerumani kumalizika, mchezo ambao Ureno iliambulia kipigo cha 4-2 siku ya Jumamosi.

Kroos Afunguka Alichokuwa Akinena na Ronaldo

Wawili hao waliwahi kucheza pamoja huko Real Madrid wakati wa enzi za dhahabu katika nyakati hizi za kisasa kabla ya Ronaldo kutimkia Italia Juventus, wiki iliyopita tumeshuhudia Sergio Ramos akiondoka Bernabeu.

Kroos Afunguka Alichokuwa Akinena na Ronaldo

“Nimecheza naye kwa misimu minne,” Kroos aliiambia Podcast ya Einfach mal Luppen.

“Tulikuwa majirani katika vyumba vya kubadili nguo kwa hiyo nilifurahi kumuona tena.

“Tuliongea kwa ufupi kuhusu mchezo, vilevile kuhusu michezo inayofuata, nilimtakia kila la heri na nilimuuliza anaendeleaje huko Italia.’

Kroos pia aliongea na mchezaji mwenzake wa zamani Pepe ambaye pia alicheza naye huko huko Real Madrid.

“Pepe pia ni mtu ambaye muda mwingine huonekana mtukutu ndani ya uwanja,” aliongeza.

“Lakini ni mtu poa sana nje ya uwanja, ni sawa kama Ronaldo.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa