Michuano ya kufuzu Kombe la dunia 2022 huko Qatar imeendelea hapo jana huku rekodi mbalimbali za magoli mengi zikiendelea kuwekwa, ambapo mataifa zaidi ya 211 yanajaribu kujitengenezea nafasi kucheza fainali hizo.

Zikiwa zimebaki takribani siku 608 mpaka pale mashindano ya kuwania Kombe la Dunia ambayo yanayoteka hisia za watu wengi duniani kuanza. Michuano hiyo itagemewa kuanza tarehe 21 Mwezi Novemba mwaka 2022. Timu za mataifa mbalimbali duniani zimeendelea jitihada zao kwa kuwania kufuzu mashindano hayo yatayofanyika Qatar kwa mara ya kwanza.

Hapo jana dunia ilishuhudia Nyota wa Liverpool, Takumi Minamino anayekipiga Southampton kwa mkopo akiwaongoza Japan katika ushindi mkubwa wa 14-0 dhidi ya Mongolia. Nyota huyo alikuwa mfungaji wa kwanza kwenye idadi ya magoli 14, akifanya hivyo dakika ya 3.

Japan na Kombe la Dunia
Japan walishinda magoli matatu dakika tatu za nyongeza!

Watu wengi walipigwa na butwaa baada ya kuona magoli matatu yakifungwa dakika tatu za nyongeza, yaani 90+1, 90+2 na 90+3. Hii yaweza kuwa rekodi mpya kuwekwa kwa mechi moja kutoa magoli matatu kwa dakika zote za nyongeza.

Mechi nyingine ilishuhudia timu ya taifa ya Canada ikiifunga timu ya taifa ya visiwa vya Cayman magoli 11-0. Mpaka sasa kuna timu nyingi ambazo zinajaribu kujihakikishia nafasi nzuri.

Bado rekodi ya muda wote ya mechi iliyotoa magoli mengi zaidi katika ya Australia na American Samoa mwaka 2011, ambapo Autsralia walishinda magoli 31-0 na mshambuliaji wao wa muda huo Archie Thompson akiweka rekodi ya kufunga magoli 13 kwenye mechi ya kimataaifa.

Je, tutegemee kuona rekodi nyingi zikiendelea kuvunjwa kuelekea fainali za Qatar? Toa maoni yako.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

kombe la dunia, Michuano Ya Kufuzu Kombe la Dunia 2022 Yaendelea Kushuhudia Magoli 10+, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa