Luka Modric amekubaliana na Real Madrid kusaini dili mpya ya mkataba rais Florentina Perez amesema.
Kumbe Modric Alisaini Dili Mpya na Madrid Kitambo
Luka Modric

Kiungo huyo wa Croatia mwenye umri wa miaka 35 ambaye alijiunga na Madrid akitokea Tottenham mwaka 2012 mkataba wake wa sasa unatarijia kuisha mwezi Juni.

Ripoti za mwezi Januari zilidai dili mpya kati ya Modric na Real Madrid tayari imeshakubalika lakini hakuna kitu chochote ambacho kilitangazwa.

Perez alithibitisha taarifa hizo siku ya Jumatano wakati wa majadiliano juu ya European Super League, wakati pia alitoa taarifa juu Sergio Ramos ambaye atakuwa nje mkataba mwisho wa msimu.

” Modric tayari amesaini au tulifikia makubaliano muda mrefu tu,” Perez alisema katika kipindi cha redio El Laguaro.

“Ramos hakupo katika hali kama hiyo, tumeongea mara nyingi lakini sijui, sitaki kumlaumu yeyote.”

Perez alikataa kuongelea hatima ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35.

“Nampenda unaweza kusema ni mwanangu, nitafanya kila ninachoweza kwaajili yake,” Perez alisema.

“Sitowaambia chochote kuhusu Sergio Ramos, tuna jaribu kumaliza msimu kisha tutaongea kinachofuata.”


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Modric, Kumbe Modric Alisaini Dili Mpya na Madrid Kitambo, Meridianbet

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa