Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti amekumbana na wakati mgumu katika kufanya chaguzi kwenye kikosi kitakachoanza dhidi ya Manchester City mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ulaya.

Los Blancos wanajiandaa kumenyana na City siku ya Jumatano katika dimba Santiago Bernabeu baada ya kupoteza mchezo wa awali kwa 4-3 nyumbani kwa City (Etihad Stadium).

Real Madrid tayari wamebeba ubngwa wa LaLiga 2021-22 ikiwa imesalia michezo minne hali iliyopelekea Ancelotti kupata wakati mgumu kuchagua wachezaji ambao wapo kwenye fomu na huenda tukashudia akiwaacha benchi wachezaji ambao wapo kwenye ubora siku ya Jumatano.

Ni wachezaji watatu pekee ambao hawana nafasi ya kucheza ambao ni Gareth Bale, Eden Hazard na Luka Jovic.

Swala kubwa hapa ni nani ataanza kati ya Rodrygo ambaye alianza wakati Casemiro alipokosa mchezo wa kwanza dhid ya Fede Valverde ambaye alicheza eneo la kiungo.

TIA JAMVI LAKO HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa