Klabu ya Barcelona imeripotiwa kufanya makubaliano ya kumsaini mshambuliaji hatari kutoka nchini Poland anayekipiga kwenye klabu ya Bayern Munich  Robert Lewandowski kwenye majira ya kiangazi.

Vyombo mbali mbali vya nchini Poland ikiwemo Interia Sport, vimedai kuwa nyota huyo wa klabu ya Bayern Munich ameshakubaliana na klabu ya Barcelona kwa mkataba wa miaka mitatu kutumikia klabu hiyo

Barcelona

Wakala wa Lewandowski Pini Zahavi, amekuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu ya Hispania La Liga kwa muda. Lakini kwa sasa vyombo vya habari vya nchini Poland vimedai kuwa makubaliano binafsi kati ya mchezaji na klabu hiyo wamefikiana, ingawa mkataba wake na Munich umebakisha mwaka mmoja.

Pia kuna vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya navyo vimeripotiwa kuwania saini ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 navyo ni Liverpool, Manchester City na PSG.

Robert Lewandowski amekuwa akicheza nchini Ujerumani tokea mwaka 2010 aliposajiriwa na klabu ya Borussia Dortmund akitokea klabu ya Lech Poznan, na amecheza kwa mafaniko kwenye klabu ya Dortmund na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Bundesliga na kombe la ligi mbele ya Bayern Munich.

Baada ya kuhamia klabu ya Munich aliendeleza makali yake, nako alifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga mara saba na ubingwa wa Ulaya.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa