Barcelona Wapo Kwenye Mazungumzo na Xavi Hernández

Barcelona wapo kwenye mazungumzo na  Xavi Hernández ya kumfanya  kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumfungashia virago aliyekuwa kocha wao Ronald Koeman jana baada ya kuwa na msimu mbovu.

Kiungo huyo wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Qatari, Al Sadd anataka kurejea kwenye viunga vya Camp Nou na kwa sasa mazungumzo yanafanyika ya kuvunja mktaba na klabu yake ya Al Sadd.

Bodi ya ya Barcelona imekuwa ikiwasiliana na Xavi kuhusu kurithi mikoba ya Koeman kwa wiki kadhaa, Barcelona watafanya maamuzi ya mrithi ya Koeman kabla ya mchezo wao wa jumapili dhidi ya Alaves ambao utapigwa Camp Nou, kwa sasa kocha wa Barcelona B anatarajiwa kuwa kocha wa muda.

Xavi ambaye amekulia kwenye akademi ya La Masia, amecheza michezo 767, ambaye kwa mara ya kwanza alitambulisha na Luis Van Gaal mwaka 1991 kwenye timu ya vijana kabla ya kuingia rasmi kwenye timu ya wakubwa mwaka 1998.

barcelona

Xavi amecheza kwa mafanikio akiwa na Barcelona ambapo aliweza kuchukua mataji 27, na kuweza kusaidia kupatikana kwa magoli 185 na pia akifunga magoli 85 kabla ya kuikacha mwaka 2015 na kwenda Qatar, Al Sadd alipocheza michezo 82 na kufunga magoli 21 na kutundika daluga na kuchukua mikoba ya kuwa kocha mkuu.


 

MCHONGO WA PESA NA CIRCUS FEVER

Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

Acha ujumbe