kiungo wa klabu ya Real Madrid Casemiro amesimama na kumtetea mchezaji mwenzake Gareth Bale baada ya mashabiki wa klabu hiyi kumzomea kwa dhihaka wakati akijaanda kuingia kwenye mchezo wa wikiendu dhidi ya Getafe.

Mshambukiaji huyo wa kimataifa kutoka Wales, aliingia kwenye dakika ya 74 akichukua nafasi ya Benzema kwenye mchezo ambao Madrid walishinda 2-0 siku ya jumamosi, na alipokuwa akijiandaa kuingia mashabiki walianza kuzomea huku Bale akiwajibu kwa kutabasmu tu.

Casemiro

Kitendo hicho kilipelekea kiungo wa klabu hiyo Casemiro kuwajibu mashabiki hao, kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo aliwataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa na heshima na mafanikio ambayo Bale ameipatia klabu hiyo.

“Mchezaji mmoja anapozomewa,  wote tumezomewa, sikubaliani na hiki kilichotokea, inabidi tumsaidie, sijapenda jinsi Bale alivyozomewa siku ile sababu yeye ni sehemu ya historia ya hii klabu, unapomzomea mchezaji kama yeye ni kama umazomea historia ya klabu, kama wote tupo pamoja, tupo pamoja.

“Nataka Bernabeu isimamishe nywele zangu kwenye bango la uwanja, tunatarajia ushirikiano wao.” Alisema Casemiro

Bale mara ya mwisho kuonekana kwenye dimba la Bernabeu kucheza ni February 2020, na amekuja kucheza tena kwenye mchezo wa juzi ambao aliingia kuchukua nafasi ya Benzema


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa