Dembele Kutangazwa Atletico Madrid.

Baada ya mshambuliaji Diego Costa kuamua kuondoka Atletico Madrid, majirani hawa wa Real Madrid walizirusha ndoano zao kule Ligue 1 wakimlenga Moussa Dembele wa Olympique Lyonnais.

Usajili wa Dembele utakuwa wa mkopo kwa nusu ya msimu uliobaki na kama mchezaji huyo ataonesha cheche zake na kuisaidia Atletico, basi atasalia Wanda Metropolitano kwa dau la euro milioni 35.

Moussa Dembele akishangilia goli lake dhidi ya Angers.

Akiwa amepachika goli 1 katika michezo 16 ya Ligue 1 aliyocheza mpaka sasa kwa msimu huu, Dembele alipachika magoli 24 katika michezo 46 (ya mashindano yote) aliyocheza msimu uliopita.

Akizungumzia usajili huo, kocha wa Atletico – Diego Simeone amenukuliwa akisema “mchakato (wa usajili) umefikia mahali pazuri. Tutathibitisha hilo (usajili wake).”

Atletico Madrid wanaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa La Liga msimu huu baada ya kuwachakaza Sevilla kwa ushindi wa 2-0 jana usiku.


MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5

Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!

INGIA MCHEZONI

16 Komentara

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Vizuri Sana dembele

    Jibu

    Safi sana dembele

    Jibu

    Usajiri makini. Familia ya dembele ina wachezaji wengi mahili

    Jibu

    Safi sana dembele

    Jibu

    Inapendeza sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Ndembele Yuko makini Sana

    Jibu

    Dembele mchezaji ninaye mkubali sana

    Jibu

    Dembele yuko poa

    Jibu

    Namkubal sana

    Jibu

    Inapendeza sana

    Jibu

    Dembele yuko fiti

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Imekaa poa

    Jibu

Acha ujumbe