Wakala wa mchezaji wa klabu ya Real Madrid Gareth Bale amethibitisha kuwa mteja wake huyo ataondoka kwenye klanye klabu hiyo msimu huu baada ya mkataba wake na mabingwa wa Hispania kumalizika.

Gareth Bale amekuwa na msimu mbaya kwenye dimba la Santiago Bernabeu kwa miaka miwili au zaidi kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na maboss wa klabu hiyo huku wakijaribu kumuweka sokoni mara kadhaa na kushindikana.

Gareth Bale

Bale anamatumaini kuwa timu yake ya taifa ya Wales itafuzu kushiriki kombe la dunia, baada ya michezo yao kusimamisha kutokana na taifa la Ukraine kuingia kwenye vita na nchi ya Urusi, na kufanya timu ya taifa hilo kutoweza kucheza michezo yake ya kufuzu.

Jonathan Barnett wakala wa Bale amethibitisha na kusema, “Gareth Bale ataondoka Real Madrid. Kurudi kwenye ligi kuu ya uingereza ni kitu kinachotarajiwa, lakini nadhani hatma yake sasa inategemea baada ya michezo ya kufuzu kombe la dunia.”

Bale tokea ajiunge na klabu ya Real Madrid amefanikiwa kushinda mataji ya La Liga 3, Copa del Rey 1, Supercopa 1, UEFA Champion League 4, UEFA Super Cup 3 na FIFA Club World Cup 3.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa