Joan Laporta: Dembele Anamakubaliano na Klabu Nyingine

Winga wa klabu ya Barcelona Ousmane Dembele hakuweza kuondoka kwenye dirisha la mwezi January, lakini raisi wa klabu hiyo Joan Laporta amethibitisha kuwa ataondoka mwisho wa msimu majira ya kiangazi.

Dembele hakuweza kuondoka kwenye uhamisho huu lakini tayari keshaamua sehemu ya kwanda baada ya mkataba wake kumalizika na miamba hiyo ya Catalunya, Joan Laporta  aliweka wazi baada kuzungumza nae na kusema hana tena mpango wa kuongeza mkataba.

Joan Laporta

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na mshindi wa kombe la Dunia akisajiriwa na klabu ya Barcelona mwaka 2017 kwa kitita cha  £100milion, kutoka klabu ya Borussia Dortmund na tokea asajiriwe hakuwa na msimu mzuri huku akitumia muda mwingi nje ya uwanja akiuguza majeruhi yake.

Joan Laporta wakati akiwa anahojiwa alinukuliwa akisema, “Dembele anamakubaliano na klabu nyingine, kwaiyo itakuwa ngumu kumuona tena akicheza kwenye klabu ya Barcelona.”

alipoulizwa tena kuhusu nafasi yake ya msimu huu  Joan Laporta allijibu, “Xavi ataamua ikiwa atampa nafasi ya kucheza tena msimu huu au asicheze kabisa huu msimu.”


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

 

 

 

Acha ujumbe