Nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona ambaye mkataba wake umekwisha kwenye klabu hiyo Ousmane Dembele kwa sasa amekubali yaishe na yupo kwenye mazungumzo ili kukamilisha makubaliano hayo.

Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, huku kukiwa na vijembe kutoka pande zote mbili sasa inaonekana mambo yanaenda kuwa safi, baada ya kuoneka mwanga kwenye mazungumzo ya makubaliano kwa pande zote mbili, huku ikitarajiwa Ousmane Dembele kusaini kandarasi ya miaka miwili kubaki kwenye viunga vya Camp Nuo.

Ousmane Dembele

Taarifa zilizopatikana mpaka sasa zinasema kuwa mazungumzo yapo kwenye hatua ya mwisho na kilichobaki ni msukumo kidogo tu ili kuweza kufanikisha dili hilo liwe kwenye mstari.

Ousmane Dembele kwa sasa ni mchezaji huru ambaye mkataba wake umekwisha na miamba hiyo ya Catalunya. Awali kulikuwa na tetesi kuwa Dembele anajianda kwenda Uingereza kwenye klabu ya Chelsea.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa