Real Madrid wameripotiwa kuweka wazi kwa Paris Saint-Germain kwamba hawatachukua hatua zozote kwa Kylian Mbappe hadi mabingwa wa Ufaransa watakapokuwa tayari kumuuza.
Hatma ya kinda huyu wa miaka 22 huko Paris inabaki kuwa mada kwenye minong’ono mingi ya soka, na mkataba wake wa sasa kusalia kule Paris uko mbioni kumalizika katika msimu wa joto wa 2022.
Ripoti ya hivi karibuni ilidai kuwa Mbappe alikuwa tayari kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na PSG kwa nia ya kujiungaa na mabingwa wa Uhispania ndani ya miaka miwili ijayo.
Real Madrid wanaonekana kutokuwa na uhakika wa kuwa na pesa zinazohitajika kupata saini ya nyota huyu wa kimataifa wa Ufaransa mwaka huu kutokana na athari za kifedha za baada ya mlipuko wa coronavirus.
Kwa mujibu wa Marca, uongozi katika wa Real Madrid umeamua rasmi kuwa hawatamfukuzia mshindi huyu wa Kombe la Dunia hadi PSG iwe tayari kuachana naye kwani kuna ‘heshima kubwa baina ya vilabu hivyo viwili’.
Mbappe, ambaye pia anaendelea kuhusishwa na Liverpool, amefunga mabao 107 katika mechi 149 katika mashindano yote kwa timu yake ya sasa tangu awasili kutoka Monaco.
Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.
Venerose
Real Madrid kuweni na subra mtampata tu
Sadick
Real Madrid haina uwezo wa kifedha kununua mchezaji wa bei kubwa kama Mbappe
Hopemwaikuka
Kwa Mbape sidhan kama itawezekana
warda
Hao PSG Wanavyoringa na huyo mmbape wao
Magdalena
Kwanini Sasa wanamuwekea kizuizi
Dorophina
Madrid wawaachie wenye ela tu wambebe mbappe
Ernest Kimeru
Naona PSG wanachelewesha deal la Mbappe kupiga mkwanja sababu utakuwa uhamisho kukata na shoka
Angelina
Hapo mchawi pesa tu
Rahma
Nice
Mwanahamisi
Nice
Sania
Hapo wanambania Mbape kuchukua mkwanja
lombo
duh
Sarah
Nice
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri pesa ndio kila kitu