Madrid Wanamfukuzia Dalot Baada ya Kumkosa Cancelo

Klabu ya Real Madrid wanaripotiwa kumtaka nyota wa Manchester United Diogo Dalot baada ya kuambiwa hawana nafasi ya kumchukua Joao Cancelo kuondoka Manchester City.

 

Madrid Wanamfukuzia Dalot Baada ya Kumkosa Cancelo

Los Blancos wanatafuta kuimarisha nafasi ya beki wa pembeni na wamekuwa wakiwafuatilia wachezaji hao wawili wa Ligi kuu ya Uingereza huku Gazeti la Mirror linadai kuwa City hawana nia ya kumuuza Cancelo na Madrid itafuata lengo la kumfuata Dalot badala yake.

Madrid Wanamfukuzia Dalot Baada ya Kumkosa Cancelo

Erik ten Hag amempa Mreno huyo nafasi katika kikosi cha kwanza ambacho amekikamata kwa mikono miwili kama kocha mkuu ambacho kwasasa kinaonekana kujiimarisha kidogokidogo.

Dalot mwenye umri wa miaka  23, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini wakuu wa Old Trafford wana chaguo la kuongeza mkataba wake kwa miezi 12 endapo watahitaji huduma yake huku Madrid wakimuhitaji.

Huenda hiyo haitoshi kumweka mchezaji huyo  Manchester kwa muda mrefu, hata hivyo, huku mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ureno akiwa hajatoa dalili zozote za kutaka kusaini mkataba wa miaka mingi.

Madrid Wanamfukuzia Dalot Baada ya Kumkosa Cancelo

Ripoti ya The Mirror inaonyesha kuwa United wanaweza kushawishiwa kutoa pesa msimu wa joto na watahitaji takriban pauni milioni 35. Ten Hag ana chaguo jingine kama beki wa kulia huku Aaron Wan-Bissaka mwenye miaka  24, akikaribia kurejea kutoka katika kipindi kirefu cha kukaa nje ya uwanja.

Acha ujumbe