Rivaldo: Koeman Anastahili Pongezi Kuliko Zidane

Legendari wa Barcelona, Rivaldo akifananisha kazi ya Ronald Koeman tangia alipochukua kibarua cha Barcelona na Zinedine Zidane akiwa Real Madrid, anasema kuwa Koeman anapaswa kupongeza zaidi.

Kwa mujibu wa Rivaldo, Koeman amefanya kazi nzuri sana na ngumu ya kuwaunganisha vijana kikosini. Aina ya uongozi wake kwa upande wake anaona kuwa inaendana sana na vijana wanavyopenda na kurahisisha mahusiano kikosini.

Rivaldo: Koeman Anastahili Pongezi Kuliko Zidane
Zidane

Wakati akimuona kama Zidane anafanya kinyume kabisa na mwezake, anasema Koeman ameweza kuviweka pamoja vipaji vya vijana na kuhakikisha bado wanaendelea kuwa na ushindani. Kwa mtazamo wake Zidane anawapa shinikizo kubwa wachezaji, kitu ambacho sio kizuri katika kuwaongoza wachezaji vijana.

Rivaldo: Koeman Anastahili Pongezi Kuliko Zidane
Rivaldo

“Wakati wopte nimekuwa nikisema kuwa namna pekee ya kuongoza vipaji chipukizi ni kutowawekea shinikizo kubwa dhidi yao, na nadhani kwa suala hili Koeman anafanya vyema zaidi. Ameweza kuwaunganisha vijana pamoja na kina Busquets, Messi, Jordi Alba. Koeman anastahili kupongezwa na kuheshimiwa kwa hilo.”

“Sifahamu nini kipo nyuma ya hili, lakini Zidane anafanya kinyume chake kwa alivyofanya kutowatumia vyema vipaji chipukizi kama Valverde, Rodrygo au Vinicius.”

Rivaldo anamtazama Zidane kama uongozi wake unakuwa katika namna ya kuwakomoa wachezaji na kwa wakati mwingine hilo linakuja kuathiri timu na siyo mchezaji pekee. Akizungumzia mfano wa makosa ambayo wachezaji wanaweza kuadhibiwa kwa faini, yeye anaweza kuwakosesha kushiriki mechi.


MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5

Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!

INGIA MCHEZONI

16 Komentara

    Koeman anajua

    Jibu

    Mmh

    Jibu

    Zidane yupo vizuri

    Jibu

    Koeman yupo vizur

    Jibu

    Koeman Yuko poa

    Jibu

    Koem kazi nzuri kafanya

    Jibu

    Norman Yuko vizuri

    Jibu

    Koeman yupo vizuri

    Jibu

    Kila kocha anakuwa na approach zake jinsi ya kuishi na wachezaji wake, Zidane anazingatia Zaidi heshima na juhudi za mtu katika kikosi.

    Jibu

    Du ni noma san

    Jibu

    Duh ni noma sn

    Jibu

    Si kweli

    Jibu

    Duh ni noma

    Jibu

    sawa

    Jibu

    Wote wanastail

    Jibu

    Duuh ni kweli janani au?

    Jibu

Acha ujumbe