Mlinzi wa klabu ya Barcelona Ronald Araujo ambaye ameongeza mkataba wa kubaki kwenye klabu hiyo yenye maskani yake kwenye jimbo la Catalunya amesema kuwa alikata offa nono kutoka kwenye vilabu vya Man utd na Liverpool sababu aliitaka kubaki sehemu anayoipenda.

Ronald Araujo mwenye miaka 23, amesaini mkataba wake siku ya ijumaa ambao utamuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2021, huku kipengere cha kuvunja mkataba wake kikiwa na thamani ya €1 billion.

Ronald Araujo
Ronald Araujo

Mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwaka 2023, klabu kubwa za Uingereza, zikiwemo Man Utd na Liverpool zilijaribu kumshawishi na kumuandalia mshahara mnono mkubwa kuliko Barcelona.

Alipokuwa anazungumza na ESPN alisema kuwa chaguo lake la kwanza mara zote lilikuwa kubaki kwenye klabu ya Barcelona, ambayo alijiunga mwaka 2018, licha ya kuwa kuna offa nono sehemu nyingine.

Nina furaha na nashawishika kubaki sehemu sahihi kwa sababu kuna mianga mingi mizuri hapa. Mara zote nilikuwa nataka  kubaki, kuna offa kunwa kutoka nje,lakini nina furaha Barcelona.

“Familia yangu inapenda hapa na mashabiki na wachezaji wezangu mara zote wamenifanya nijisikie nyumbani.

“Nina shukuru kwa juhudi ambazo klabu imefanya. wote tumechangia kidogo kufanikisha makubaliano, ambayo tulikuwa tunataka.

“Kuhitajika EPL hakukunizuzua. Nashawishika na kile nitakacho. Ni kweli pesa ni sababu, lakini kwangu ni tofauti, pesa sio kitu muhimu. Nina furaha Barcelona.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa