Safari ya Real Madrid Kutoka Galacticos

Real Madrid walikuwa na sera yao ya Galacticos chini ya Rais Perez alivyoingia madarakani kwa mara ya kwanza 2000-06, aliamini zaidi kwenye kununua Mastaa

Kwa kipindi chake cha kwanza kabla ya kung’atuka aliwanunua Zinadine Zidane, Ronaldo De Lima, David Beckham, Luis Figo, Michael Owen na Robinho, kipindi hicho walibeba UEFA moja na Ligi mbili.

Baadae Madridistas walimpinga sana Perez, waliamini hakuwa anasajili kwa mahitaji ya kikosi wala hakuwa anajali wanacheza vipi bali aliwaza zaidi biashara, akalazmika kubwaga manyanga

Aliporejea kwa mara ya pili 2009, alisajili wachezaji wakubwa tena akiwemo Cristiano Ronaldo, Kaka, Benzema, Alvaro Alberoa, Ozil, James, Isco na Mastaa wengi kikosini.

Awamu ya pili hii amebeba makombe mawili ya Ligi na UEFA nne, lakini safari hii Perez alijuwa kuwa wachezaji alionao hawatokuwepo kwa miaka mitano mpaka sita ijayo ndipo alipokuja na plan maalum kupitia La Fabrica, academy hii ya Real Madrid.

Perez akaanza kuzunguka duniani kote kupitia mawakala wake na kusaini wachezaji Makinda wenye ubora mkubwa sana kisha kuwatoa kwa mkopo, pale Brazil waliwasaini Rodrygo, Vinicius Jr na Reiner Jesus.

Kule Uruguay walimnasa Kinda Federico Valverde, Norway walimchukua Martin Odergard, kinda Takefuso Kubo wa Japan, Sergio Reguillon na wengine wengi wakiwapeleka kwa mkopo kupata muda wa kucheza.

Katika ile project ya miaka mitano au sita iliopita ni sasa imeanza kuwalipa, Odeergard amerejea na huenda akarithi viatu vya Modric, Valverde ametulia kuvaa viatu vya Kroos au Case, Reguillon yupo Spurs akirejea huenda ataanza

Rodrygo Goes na Vini Jr nao wameshaanza kupata dakika za kutosha kikosini, wakijaribu kuvaa viatu vya Gareth Bale na Ronaldo, huku wengi wakimsubiri Takefuso Kubo alie kwa mkopo Villareal na Dani Ceballos kutoka Arsenal.

Huu ni mpango kazi wa Real Madrid na Perez kwenye maisha mapya kutoka Galacticos mpaka kuzalisha watoto wadogo na kufikia sehemu kubwa, ni suala la muda tu, ulikuwa ni mpango kazi tangu 2014 na sasa unatimia.


UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

24 Komentara

    Watu na sera yao duuh noma sana

    Jibu

    Natumain soon mpango wa perez utakamilika Kwan kuna kila dalili zinaonyesha watoto wameshakwiva katika kupambania namba katika cha la madrid hapo naona Kuna uwezekano mkubwa wa Madrid kuwa rejesha na pamoja na kupata combination nzuri ambayo itawaunganisha pamoja na kutengeneza timu yenye ushindan ndani na nje katika soka la hv sasa

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Hatari sana

    Jibu

    I hope mambo yataenda kama yalivyopangwa

    Jibu

    Plan kali kwa madrid itawapa mataj kwa muda mrefu

    Jibu

    Kwakweli lazima.uwe na maono ya mbari na ndio maana kikosi lilikuwa bora hadi sasa #meridianbett

    Jibu

    Duuh atari sana

    Jibu

    Plan kali Mambo yatakuwa mazur tyu

    Jibu

    watu wana ndoto za kwenda mbali

    Jibu

    huu hupango madrid hutawapa manufaa makubwa zaidi

    Jibu

    Kwa madrid hapo wameteleza

    Jibu

    Ndoto zake naamini zitafanikiwa kwa asilimia zote maana naona vijana wapo vizuri wameiva ipasavyo

    Jibu

    Watu wanaona mbali!!!

    Jibu

    Mpango mzuri ila kama Ronald ataweka sokeni ninaona bora real Madrid wamchukue tena mana hapo panamfaa zaidi

    Jibu

    Madrid ilikua moto kipind hiko ila zizou anatakiwa airudishe tena

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Madrid ilikua enz hizo

    Jibu

    Madrid ni moto

    Jibu

    Asante kwataarifa meridianbet

    Jibu

    Mpango wao madrid upo vizuri inawekana kuwafikisha mbali

    Jibu

    Madrid ni moto wakuotea mbali

    Jibu

    Asante kwa taharifa

    Jibu

Acha ujumbe