The Miracle of Liverpool in Istanbul

Mzee mmoja shabiki sugu wa Liverpool alinyanyuka na kutoka uwanjani. Akasogea hadi ‘Pub’ iliyokuwa jirani, akaagiza glasi ya ‘Whisky’ kupooza koo lake lililokuwa linaungua moto, kisha akawasha sigara kutuliza mapafu yake yaliyokuwa yakiumia kwa kukosa hewa. Alipomaliza akashika njia na kurudi uwanjani.

Aliiendea siti yake kisha akanyanyua mikono yake juu na kuishusha chini. Akarudia tena mara ya pili na ya tatu, kisha jirani yake wa kulia na kushoto wakamfuata. Dakika mbili mbele jukwaa zima lilimfuata. Taratibu akaanzisha ‘goma’ la ‘Fields of Anfield Road’. Hapo ndipo mashabiki wa Liverpool walivaa ule ukichaa wao halisi. Wakaimba kwa hisia kali sana. Hadi waturuki na ukichaa wao waliwashangaa. Yaani mpo nyuma tatu kwa bila halafu mnaimba hivi?

Kule chumbani Rafael Benitez alimaliza kutoa maelekezo. Kisha akamuachia Steven Gerrard amalize kabla hawajarudi kipindi cha pili. Gerrad alisimama katikati ya chumba akasema, “Hapa sizungumzi kama captain, bali nazungumza kama shabiki wa kutupwa wa Liverpool. Mnawasikia hao wanaopiga hizo kelele? Wamesafiri kwa basi hadi kufika hapa, wamechoka, hawajalala toka jana. Tumeshafungwa tatu lakini bado hawajakata tamaa. Hao ndio Liverpool. Twendeni tukailipe imani yao kwetu. Hata ikibidi tuiache miguu uwanjani. Sisi ndio Liverpool. Tunaweza.”

Waliporejea kipindi cha pili, Benitez akafanya mabadiliko. Akamtoa Steve Finnan na kumuingiza Dietmar Hamman. Liverpool wakatoka kwenye 4-4-1-1 na kuingia 3-5-2. Hapo ndipo balaa lilipoanzia. Kumbuka kule jukwaani goma la fields of Anfield linaendelea kungurumisha.

Hapo ndani anatajwa ‘mr. Liverpool’ Billy Shanky na masikitiko ya kifo chake. Anatajwa Bob Paisley na maajabu ya Roma ya mwaka1977, anatajwa Kenny Daglish na heshima yake. Inapofika hapo haiwi soka tena bali mapambano ya uhai na kifo. Kila mchezaji wa Liverpool anakuwa radhi kupasuka kichwa, kutoka macho na kuvunjika mguu kwa ajili ya Liverpool, hisia zinakuwa kali sana.

Ndipo hapo dakika ya 54 John Riise anamimina krosi inaishia kichwani mwa Gerrard. Ndipo hapo dakika ya 56…

ITAENDELEA…


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

26 Komentara

    Liverpool walifanya comback ya hatarii

    Jibu

    This is anfield

    Jibu

    Makala nzui bora uhondo ungeisha leo leo

    Jibu

    hii ndio Liverpool

    Jibu

    Kikosi cha Liverpool kipo vizuri sana

    Jibu

    Naikubali Liverpool wakiamua kufanya yao washindwagi

    Jibu

    Hii Ni bonge la makala

    Jibu

    Liverpool wapo vinzur

    Jibu

    Liverpool wamejipanga

    Jibu

    Hao ndo mashabiki kindakindaki

    Jibu

    Liverpool club kubwa naikubali hatar

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Liverpool iko vizuri sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Liverpool wapo vizuri

    Jibu

    Liverpool safi sana

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Liverpool wazee wa kupindua Meza

    Jibu

    Liverpool tishio

    Jibu

    Yalikuwa maajabu kweli kweli

    Jibu

    Good

    Jibu

    liverpool walifanya kazi kubwa sana

    Jibu

    Good news

    Jibu

    liverpool wapo vizuri

    Jibu

    Hii ndio liverpool

    Jibu

    Mambo ni moto

    Jibu

Acha ujumbe