Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amesema kuwa Ousmane Dembele lazima aamue ikiwa anataka kubakia kwenye klabu au lah kutokana na tetesi zinavyozunguka kuhusu hatma yake.

Ousmane Dembele alitarajiwa kuondoka kwenye klabu ya Barcelona kwenye dirisha la  usajiri mwezi januari, wakati klabu na viongozi wake wakiwa wanashinikiza eidha asaini mkataba mpya au aondoke kwenye klabu hiyo.

Xavi
Xavi Hernandez

Dembele tokea asajiriwe na klabu ya Barcelona kutokea klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund, hakuwa na wakati mzuri kwani alitumia muda mwingi akiwa na majeruhi kuliko uwanjani, na tangia atengemae chini ya Xavi amekuwa akionyesha kiwango bora sana na  kuwa sehemu ya wachezaji tegemezi kwenye klabu hiyo.

Wakati sintofahamu ya wapi atakwenda, Xavi amemuomba mchezaji huyo kuweka wazi hatma yake ikiwa anataka kusalia kwenye klabu hiyo au lah.

“Namuona anafuraha sana, anajuhusiha kwenye mipango tangia nimefika hapa, sina la malalamiko kuhusu yeye, ni swali kwa  Ousmane kuweza kujibu kuhusu hatma yake, mimi niko wazi kwenye hilo.

“Anafanya mabadiliko makubwa kwetu, anatusaidia jinsi anavyocheza, ni mtu muhimu kwa sababu jinsi ninavyotaka tucheze,  kwenye mpira wa pasi fupi fupi ni mzuri,” alisema Xavi.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa