Kati ya vitu ambavyo pengine havikutarajiwa mwanzoni kwa msimu huu wa LaLiga, ni kuiona Barcelona kwenye ubora wake.

Mashabiki na wapenzi wa soka tuliamini huu ni msimu wa kuijenga Barca chini ya Koeman lakini sio Kutwaa ubingwa.

Kadiri siku zinavyosonga mbele, mambo yanakuwa tofauti. Barcelona imetoka kuwa “underdogs” na sasa ni “tittle challengers”.

Mchezo dhidi ya Real Valladolid Jana usiku, umetoa taswira mpya ya msimamo wa LaLiga kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Licha ya timu zote kupambana kusaka goli, juhudi zao ziligonga miamba kila mara.

Ila asikwambie mtu, dakika 1 ni kubwa sana na kwenye soka, mpira haumaliziki bila kipenga cha mwisho cha mwamuzi.

Ousmane Dembele kunako dakika ya 90 aliwainua mashabiki wa Barca na kuipatia timu Hiyo pointi 3 muhimu.

laliga - dembele alishangilia pointi 3 muhimu kwa Barca
Dembele alishangilia pointi 3 muhimu kwa Barca

Ushindi wa Barcelona dhidi ya Valladolid na kufungwa kwa Atletico Madrid (1-0 dhidi ya Sevilla) wikiendi iliyopita. Kunaipaisha Barca Mpaka Nafasi ya 2 wakiwa na pointi 65, pointi 1 pungufu ya Atletico kwenye msimamo wa LaLiga msimu huu.

Hii ni ishara kuwa, ubingwa wa Real Madrid msimu uliopita sambamba na Nafasi ya Atletico vyote vipo matatani. Barca wanapiga hodi kwenye ubingwa wa LaLiga msimu huu.

Nani atamfunga Paka kengele? Wikiendi hii Barcelona atachuana na Real Madrid, pengine mchezo huu utaamua Nani anausogelea ubingwa kwa ukaribu zaidi msimu huu. Mambo ni moto huko nchini Hispania.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

laliga, LaLiga: Barcelona Wanapiga Hodi!!, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa