Liverpool na PSG Zapigania Saini ya Yan Diomande

Klabu ya Liverpool imeanza hatua za awali za kutaka kumsajili winga kijana Yan Diomande huku ikikumbana na ushindani mkubwa kutoka kwa Paris Saint-Germain inayomtaka pia nyota huyo mwenye umri wa miaka 19.

Liverpool na PSG Zapigania Saini ya Yan DiomandeVyanzo vinaeleza kuwa viongozi wa Liverpool wanataka kukamilisha dili hilo kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, lakini mazungumzo bado yako katika hatua za mwanzo kati ya klabu na mawakala wa mchezaji huyo. Mbali na PSG, Bayern Munich nayo imehusishwa na mbio za kumuwania Diomande.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Klabu ya RB Leipzig inapendelea kumbakisha Diomande kwa angalau msimu mmoja zaidi, ingawa inaweza kusikiliza ofa zinazokadiriwa kufikia euro milioni 100 kwa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye ana mkataba hadi mwaka 2030.

Liverpool na PSG Zapigania Saini ya Yan DiomandeLiverpool imeongeza nguvu katika harakati za kumpata Diomande kufuatia kuondoka kwa Mohamed Salah, huku ikitafuta kuongeza kasi na ubunifu zaidi katika safu ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao.

Liverpool na PSG Zapigania Saini ya Yan Diomande“Liverpool wanaamini Diomande ni mmoja wa washambuliaji vijana bora sokoni kutokana na umri wake, uwezo wa kucheza pande zote za ushambuliaji na nafasi kubwa ya kuendelea kukua kisoka,”

Liverpool na PSG Zapigania Saini ya Yan DiomandeDiomande alikuwa na msimu mzuri nchini Ujerumani baada ya kufunga mabao 13 na kutoa pasi 10 za mabao katika michezo 36 aliyocheza mashindano yote tangu ajiunge akitokea Leganés mwaka jana. Mbali na Diomande, Liverpool pia imewatazama Anthony Gordon, Bradley Barcola, Jarrod Bowen pamoja na Mohammed Kudus kama chaguo mbadala katika eneo la ushambuliaji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.