Mchezaji wa zamani na Manchester United na kocha wa Derby County Wayne Rooney ameachana na klabu hiyo leo, waraka wa klabu umethibitisha hilo.

Waraka wa Derby County ulisomeka “Wayne Rooney ameitaarifu klabu ya Derby County Football Club, kwamba anahitaji kuachia ngazi ya nafasi ya ukocha wa kikosi cha kwanza ili apate muda wa kupumzika haraka iwezekanvyo.”

Wayne Rooney

Wayne Rooney alijiunga na klabu ya Derby County kama mchezaji, baadae akawa kocha mchezaji kabla ya kupewa majukumu ya kuinoa kabisa na kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

Rooney alikuwa na wakati mzuri tangu achukue majukumu ya kuinoa klabu hiyo. Ijapokuwa, kutokana na makosa yaliofanywa na mmiliki wa klabu, ilipelekea klabu ya Derby kupunguzwa alama 21 msimo uliopita.

Japo inaonekana Wayne Rooney amefanya maamuzi ya haraka na hayakutarajiwa, zimeanza kuzuka tetesi kuhusu uwelekeo wake kuwa kuna dalili wa yeye kurudi tena kwenye moja ya klabu ya Championship.


 

ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa