Michezo ya Regular Season kunako NBA imekamilika na sasa macho yote ni kwenye Play-Offs, LeBron James aokoa jahazi la Lakers akitoka kwenye majeruhi.

LA Lakers walikuwa uwanjani kuchuana na Golden State Warriors katika mchezo wa Play-in tournament. Huu ni mchezo ambao uliozikutanisha timu 2 zenye upinzani mkubwa kwenye NBA na safari hii zilikuwa zinachuana kuwania nafasi 2 zilizobaki kwenye msimamo wa Western Conference.

LeBron James, LeBron James Aivusha LA Lakers Kunako NBA Play-Offs, Meridianbet
James akipachika mpira wa pointi 3 muhimu kwa Lakers vs Warriors.

Baada ya kukosekana kwenye michezo kadhaa ya Laker, LeBron James alipachika pointi 3 muhimu zikiwa zimesalia sekunde 58 mchezo huo kumalizika. Ushindi wa pointi 103-100 umewatosha Lakers kufuzu hatua ya mtoano na sasa watachuana na Phoenix Suns katika mchezo wa kwanza siku ya Jumapili.

Licha ya Stephen Curry kupachika jumla ya pointi 37 kwenye mchezo huo, hazikuwatosha Warriors kufuzu na badala yake watachuana na Memphis Grizzlies kwenye mchezo ambao mshindi ataungana na timu zingine 7 zilizofuzu kucheza NBA Play-Offs kwa upande wa Western Conference.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

LeBron James, LeBron James Aivusha LA Lakers Kunako NBA Play-Offs, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa