Nyota wa klabu ya Olympique de Marseille Dimitri Payet atakosa michezo yote iliyobaki kumalizia msimu huu baada ya kupata majera ya mguu kwenye mchezo wa UEFA Europa Conference League dhidi ya Feyenoord siku ya alhamisi.

Dimitri Payet amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu huu na kufanikiwa kufunga magoli 16 na kusaidia kupatikana mengine 13 kwenye michezo yote, huku akiiongoza Olympique de Marseille kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1.

Dimitri Payet
Dimitri Payet

Olympique de Marseille safari yao kwenye mashindano ya UEFA Europa Conference League imehitimishwa na Feyenoord kwenye mchezo wa nusu fainali kwa uwiano wa magoli 2-3, lakini Marseille wanaweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa ulaya ikiwa tu watashinda michezo yao yote iliyobakia.

“Dimitri Payet anasumbuliwa na tatizo la msuli baada ya kumfanyia vipimo vya kawaida.” Waraka wa klabu uliotolewa kuhusu hali yake. “Matibabu tayari yameshaanza, lakini tunatarajia kupona kwake baada ya ligi kuisha.”

Marseille amebakisha michezo mitatu ili amalize ligi michezo hiyo atacheza dhidi ya  FC Lorient, Stade Rennais FC na RC Strasourg, akifanikiwa kushinda yote au miwili kati ya hiyo basi atakuwa amejihakikishia kucheza ligi ya mabingwa ulaya.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa