Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain Lionel Messi ataukosa mchezo wa siku ya jumatano ambao watasafiri kwenda kuwafuata Angers kutokana na majeruhi, mchezo ambao wanaweza kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1.

Lionel Messi anatatizo la tendoni kwenye mguu wake wa kushoto, kulingana na taarifa iliyotolewa na klabu ya PSG, nyota huyo wa kimataifa kutokea Argentina ambaye alisajiriwa na klabu hiyo kwenye majira ya kiangazi kutokea Barcelona, mpaka sasa amekosa michezo kadhaa kutokana na majeruhi na Uviko-19 kwenye klabu hiyo.

Lionel Messi
Lionel Messi

PSG iko kileleni mwa ligi kwa alama 15 zaidi ya klabu inayomfuatia Marseille, huku klabu ya PSG wanakwenda kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa wake wa kumi.

Ikiwa PSG atafanikiwa kumfunga Angers na Marseille anayeshika nafasi ya pili akatoa sare nyumbani dhidi ya Nantes, basi Les Parisiens (PSG) watakuwa sawa na Marseille na Saint-Etienne kuwa klabu zilizochukua makombe mengi Ufaransa.

Kiungo Marco Verratti na mlinzi Presnel Kimpembe watakosa mchezo huo kutokana na majeraha, wachezaji wote watatu watafanyiwa tena vipimo kabla ya mchezo wa PSG dhidi ya Lens wikiendi.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa