Mathias Pogba ambaye ni ndugu yake na kiungo wa kamataifa wa Ufaransa na mchezaji wa klabu ya Juventus Paul Pogba amekana kuwa sehemu ya watu wanaomhujumu ndugu yake leo.

Mwanasheria wa Mathias Pogba, Richard Arbib kwenye waraka alisema kwamba wakala wake alitaka kueleza kwa unyenyekevu kwamba yeye alikuwa hajui chochote kwenye jaribio la hujuma dhidi ya kaka yake Paul Pogba.

Mathias Pogba, Mathias Pogba Akana Kumuhujumu Ndugu Yake, Meridianbet

Majaji wawili walichaguliwa wiki iliyopita ili kuchunguza shutuma ambazo mshindi wa kombe la dunia alikuwa amelengwa na ndugu yake na rafiki zake wa utotoni.

Arbib alisisitiza kuwa Mathias Pogba hataki kitu kingine zaidi chochote zaidi ya kuweka sama mambo na kaka yake. Muendesha mashitaka wa jijini Paris alifungua kesi hiyo mwezi mmoja uliopita kwenye jaribio la hujuma, ambalo kwa sasa linashughukiwa na idara ya kupambana na rushwa.

Mamlaka ya Ufaransa wanachunguza shutuma ambazo Pogba ndio mlengwa wa hujuma ambazo zimepangwa na kaka yake na rafiki zake wa utotoni ambao walikuwa wanahitaji kulipwa kiasi cha euros 13 million.

Pogba alishawai kufuatwa na kikindi cha watu kwenye uwanja wa mazoezi wa Juventus kuhusu madai yao ya pesa huku ndugu yake  Mathias Pogba akiwa mmoja wapo, kulingana na taarifa ya France-Info radio.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa