Baada ya Mchezaji wa Manchester United kuonesha kiwango kizuri sana katika mechi ya robo fainali ya mkondo wa Kwanza dhidi ya Roma, Lindelof amempongeza mchezaji huyo na kumtaka asalie United.

Lindelof alidai kuwa Cavani amekuwa mhimili mzuri sana katika kikosi cha Man United na uchezaji wake mzuri katika mechi hiyo ulikuwa muhimu sana. Cavani alicheza kwa kiwango kizuri sana na akafanikiwa kufunga magoli mawili na kuweka pasi za magoli 2.

Cavani alitumia ujuzi wake pamoja na ukomavu wake kwenye mpira na kujihakikishia mchezo mzuri. Kumekuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo hana uhakika wa kusalia United kutokana na kuwa na wakati mgumu katika mji wa Manchester.

Lindelof alisema hayo katika mahojiano na kipindi maalum cha Man U TV, alidai kwamba kwa namna mechi hiyo ilivyokuwa na kipindi kizuri kwa United, alitamani sana kungekuwepo na mashabiki katika mechi hiyo.

Hivi karibuni kocha wa kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solkjaer alieleza kuwa anatamani Cavani kusalia United na atafanya awezalo kuhakikisha kuwa mchezaji huyo anasalia United.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa