Kunako EPL leo mchana, Liverpool wamejikuta wakisuluhu mchezo wa 2 mfululizo ndani ya wiki 1. Kuna nini kunako kikosi cha Jurgen Klopp?

Jumatatu mabingwa hawa watetezi wa EPL walijikuta wakipoteza pointi 3 muhimu licha ya kuongoza kwa goli 1 dhidi ya Leeds United. Dakika ya 87, Diego Llorente akapindua meza na kugawana pointi 1 kila mmoja.

Haitoshi, leo mchana wakiwa Anfield, goli la Mo Salah kunako dakika ya 3 halijatosha kuwapa ushindi Liverpool. Akitokea benchi, Willock ambaye aliwapa ushindi muhimu Newcastle dhidi ya West Ham United kwenye mchezo uliopita, amerudia tena kwenye mchezo wa leo baada ya kupachika goli la kusawazisha kunako dakika ya 95.

Matokeo ya sare 2 mfululizo, yanaendelea kuyaweka rehani matumaini ya Jurgen Klopp kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Hakika kule Anfield ni mwendo wa Kampa, kampa tena!! Kituo kinachofuata kwa majogoo wa uingereza ni Old Trafford wikiendi ijayo, hali itakuwaje?


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Liverpool, Liverpool, HAMJIFUNZI? Kampa Kampa Tena., Meridianbet

CHEZA HAPA

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa