Liverpool inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ikiwa ugenini usiku wa kuamkia leo imetwaa pointi tatu muhimu mbele ya Burnley jambo ambalo limewapa matumaini ya kuweza kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa  Turf Moor ulisoma Burney 0-3 Liverpool.

Liverpool Celebrate

Ni Robert Firmino dakika ya 43, Nathaniel Phillips dakika ya 52 na Alex Oxlade Chamberlain dakika ya 88 walipachika mabao kwa Liverpool.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha alama 66 ikiwa nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 37 na Burnley ipo nafasi ya 17 na pointi 39.

Liverpool-

Liverpool kazi ya kushinda mchezo wake mmoja wa mwisho uliobaki ili kuweza kumaliza katika nafasi hiyo ya nne kwa kuwa mshindani wake Leicester City ambaye yupo nafasi ya tano naye pia ana pointi 66 hivyo akipoteza na mpinzani wake akashinda atashushwa hapo alipo.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Liverpool, Liverpool Matumaini Kumaliza 4 Bora EPL, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa