Liverpool wameripotiwa kuwa wamewasiliana na RB Leipzig kuwa kwa sasa hawataendelea na dili la uhamisho la beki wa klabu hiyo Ibrahima Konate katika dirisha la uhamisho la msimu ujao wa joto.

Wakati Jurgen Klopp akisaka angalau nyongeza ya nguvu kwenye safu yake ya Ulinzi ambayo ilikubwa na shida ya majeraha, Konate aliaminika kuwepo kwenye rada ya Liverpool pale dirisha la uhamisho linapofunguliwa.

Liverpool Kwa Kounate.

Julian Nagelsmann tayari atakuwa anapunga mkono wa kwaheri kwa Dayot Upamecano baada ya Bayern Munich kukubaliana na dili la mlinzi huyu wa Ufaransa, huku Liverpool na Manchester United wakitajwa kuwa kwenye kinyang’anyiro cha saini ya Konate.

Kwa mujibu wa ripoti, Leipzig waliwasilana na Liverpool ili kufahamu nia yao ya kumsajili staa huyo, lakini wamewaambia kuwa hawatarajii kufanya uhamisho wa staa huyo mwenye miaka 21.

Konate pia alisema masuala ya uhamisho wake ni minong’ono tu ambayo yeye mwenyewe amechoka kuisikia, alisema hayo akiwa kwenye majukumu ya kitaifa na kikosi cha vijana cha Ufaransa.


 

INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

Liverpool, Liverpool Watemana na Dili la Konate, Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa