Beki wa Liverpool, Dejan Lovren yupo mbioni kujiunga na club ya Zenit St. Petersburg kwa ada ya pauni 11 milioni.

Lovren alijiunga na Liverpool akitokea Southampton mwezi July 2014 kwa ada ya uhamisho wa pauni 20 milioni. Kwa miaka sita aliyokaa Merseyside amehusika kwenye ubingwa wa ligi kuu walioutwaa Liverpool na taji la club bingwa barani Ulaya.

Lovren Kutua Zenit, Lovren Kutua Zenit, Meridianbet

Hata hivo, Mcroatia huyu mwenye miaka 31 amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Virgil Van Djik, Joe Gomez na Joel Matip. Msimu huu Lovren amecheza jumla ya michezo 15 pekee katika mashindano yote.

Lovren Kutua Zenit, Lovren Kutua Zenit, Meridianbet

Liverpool wapo tayari kumuacha Lovren aondoke iwapo atafikia makubaliano binafsi na club ya Zenit. Lovren amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na majogoo wa jiji na bado wana kipengele cha kumuongezea mwaka mmoja iwapo watahitaji kufanya hivo.


Kwa sababu ya thamani ya pesa yako, kwa kila muamala unaofanya wa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet unapata 5% bonasi.

Soma Zaidi

48 MAONI

  1. Lovren mchezaji mahiri aliyetumikia Liverpool ipasavyo tunategemea akaonyeshe maajabu zaidi zenit.

  2. Croatia ina vipaji vingi sana. Lakini wakati anacheza mara kwa mara beki yao iliruhusu magoli mengi sana #meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa