Ni saa 5:15 Asubuhi kwa saa za Kusini Mashariki mwa Bara la Ulaya, Desemba 8 mnamo 1991, kwenye Kijiji kidogo cha Modrici huko Jamhuri ya watu wa Croatia ambapo zamani ilifahamika kama Yugoslavia chini tu ya milima ya Velebit.

Alikuwepo Luka Modric Snr, Babu yake Kiungo Luka Modric akichunga ng’ombe ila ghafla sana alizungukwa na kundi la wanajeshi wa Serbia, katikati ya vita kubwa iliyofahamika kama YUGOSLAVIAN CIVIL WAR, Serbia akiwa mbabe haswa.

Babu yake Luka Modric alipigwa risasi na kuburuzwa kwenye mkokoteni wakati ambao Modric ana miaka sita tu na Dada yake Jasmine wakichungulia kwa mbali walipojificha, Babu amefariki na lilikuwa tegemeo kubwa la Modric, huku wazazi wao wakifanya kazi kiwandani.

Katikati ya vita Modric na familia yake baada ya kifo cha Babu walilazimika kukimbia Mji, wanakimbia wakati ambapo Modric akitazama nyuma anaona familia nyingi zinateketea, watoto na Wamama wanakufa, alikimbia na familia kwa kadri ambavyo miguu iliweza kumbeba.

Modric alitazama kile kijiji kutokana na sehemu ambayo ndoto zake za kuwa Mwanasoka zilizaliwa pamoja na Rafiki zake, sehemu ambayo Babu yake ambaye ndiye marehemu waliongea mengi na Mjukuu wake, hatimae leo Modric anapakimbia kutokana na vita.

Luka
Modric akiwa mtoto

Walikimbilia kwenye mji wa Zadar, sehemu ambayo Mudumu aliwapokea wakiwa wamechoka mno, Modric akiwa na majeraha makubwa na Wazazi wamechoka haswaa, waliomba kwanza chumba cha kupumzika, walilazimika kuishi kwenye hotel kwa zaidi ya miaka saba wakati vita inaendelea kupigwa.

Luka
Modric na Wazazi wake

Ni kuanzia kwenye hotel hiyo iliyoitwa HOTEL 12, ndipo the ndoto za Modric zilizidi kuchipua, alicheza mpira akiwa na shin pads zenye picha za wachezaji wa Kibrazil, wakati wa jioni kwenye parking za hotel hiyo, alipambana kuishi kwenye ndoto yake hata wakati wa magumu makuu.

Miaka sasa imepita tangu 1991, yupo wapi leo Modric, ni Mshindi wa Ballon d’or, ana medali ya kombe la dunia, ana UEFA nne na ni moja kati ya viungo bora sana duniani.

Luka Modrick Alikimbia Vita, Akatwaa Ballon d'Or


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Luka, Luka Modric Alikimbia Vita, Akatwaa Ballon d’Or, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa