Kikawaida, dirisha la usajili linakuwaga na sajili konki kuelekea mwishoni mwa usajili. Romelu Lukaku, Erling Haaland, Harry Kane wanateka vichwa vya habari.

Kane amegoma kurejea mazoezini na kikosi cha Spurs kwa kile anachodai kuwa, alikuwa na makubaliano na klabu hiyo (tangu msimu uliopita) kuwa ataruhusiwa kuondoka klabuni hapo endapo timu zitajitokeza kumuhitaji.

Man City wamejitosa kwa kutoa dau la £120M ambalo Spurs walilikataa mchana kweupe. Spurs wameweka thamani ya £160M kwa timu inayomtaka Kane na hakuna aliyeisogelea gharama hiyo.

Chelsea wameambulia patupu katika harakati zao za kutaka kumsajili Erling Haaland kutokea Borussia Dortmund. Kwa hali ilivyo, Haaland ataendelea kuwepo Dortmund msimu ujao lakini ifikapo Juni 30, 2022 – timu zitaweza kumnunua kwa dau la £75M tu.

Lukaku, Lukaku Kuwapiga Tafu United Sokoni., Meridianbet

The Blues wamehamishia majeshi yao kwa Romelu Lukaku. Imeripotiwa kuwa, Chelsea walitoa dau la €100M pamoja na Marcus Alonso lakini Inter walikataa. Sasa Chelsea wanajipanga kupeleka dau nono zaidi linalokadiriwa kuwa ni kati ya €120-130M.

Katika hili, Man United wanaangalia mchakato huu kwa jicho la kichumi. Endapo Lukaku ataondoka Inter, United watapaswa kulipwa kiasi cha pesa kama ambavyo walikubaliana na Inter (2018) wakati walipomuuza mchezaji huyo kwenda Inter.

Inakadiriwa kuwa, Inter itapaswa kuilipa United takribani £43M kwa usajili wowote watakaoufanya kwa Romelu ikiwa ni sehemu ya kipengele cha mkataba kati ya timu hizo. Pesa hizi ni zile ambazo Inter inaripotiwa kutomaliza kuilipa United ada nzima ya usajili wa mshambuliaji huyo (£73M).

Kama Chelsea watafanikiwa, United wapo kwenye nafasi nzuri ya kutengeneza pesa kupitia Chelsea na Inter Milan na hivyo kuimarisha zaidi kikosi chao.


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa