Usiku wa jana, Juventus walikutana na Parma na huwezi amini matokeo ya mechi hiyo yaliamuliwa na magoli matatu kutoka kwa mabeki wa timu hiyo.

Juventus ililazimika kushinda mechi ya jana ili ijihakikishie kurudi ‘Top 4’ na kucheza UEFA Champions League msimu ujao. Mechi ilianza kwa timu zote kushambulia kwa nyakati tofauti. Huku Dybala na Ronaldo wakikosa magoli ya wazi.

Mpira wa kufa wa Gaston Brugman dakika ya 25 ukawapa goli la kuongoza Parma, mpaka pale dakika ya 43 ambapo mlinzi wa kulia wa Juventus Alex Sandro alipofunga goli la kuisawazishia timu yake.

kipindi kilipoanza Juventus walionekana kushambulia sana lango la Parma, na mnamo dakika ya 47, Sandro yule yule akamalizia kwa kichwa ‘cross’ ya Cuadrado. Kabla ya beki wao mwingine wa kati, De Ligt kumalizia goli la kichwa dakika ya 68.

Juventus

Kutokana na matokeo hayo mabingwa hao watetezi wa Serie A wamerudi nafasi ya tatu, wakiwa na alama 65 juu ya Atalanta wenye alama 64 na mchezo mmoja mkononi, ambao watacheza dhidi ya wakongwe Roma jioni ya leo.

Kwa kawaida Serie A hutoa timu nne za juu kwenda kucheza UCL, lakini Juventus msimu huu walionekana kusuasua na wana hati hati ya kupoteza ubingwa wa ligi hiyo.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

juventus, Mabeki Warudisha Matumaini Juventus, Meridianbet

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa