Nyota wa timu ya taifa ya wanawake ya Jamhuri ya Ireland, Megan Campbell bado anaendelea kuuguza jeraha lake la enka lililomuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kiasi cha kutishia kumaliza career yake.

Campbell amekua nje ya uwanja tangu mwezi January baada ya kujeruhiwa akiitumikia klabu yake ta Manchester City katika ligi ya wanawake ‘WSL’.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amekua akiabdamwa na majeraha ya mara kwa mara na hali hiyo inaridisha nyuma maendeleo yake kisoka.

Majeraha ya enka yanayomsumbua hivi sasa aliyapata katika mechi ya kwanza kabisa ya msimu wa 2019/20 pale walipomenyana na Tottenham Hotspur hali iliyopelekea kufanyiwa upasuaji katika enka yake ya mguu wa kulia.

Campbell hivi sasa anaendelea vizuri na lengo lake ni kurejea uwanjani mapema iwezekanavyo Ili aweze kuisaidia timu yake ya taifa ya Ireland ifuzu kushiriki mashindano ya Ubingwa wa Ulaya yatakayofanyika mwaka 2022.

 

 

46 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa