Mpira wa miguu ni miongoni mwa michezo rafiki sana duniani. Mchezo huu unapendwa, kuheshimiwa na idadi kubwa sana ya mashabiki. Kuna wakati mwingine huibua hisia nzito pale unapoona timu unayoishangilia na kuipenda inafanya vizuri na kuona wachezaji wakiwa na furaha ya kushinda taji fulani. Leo tunakuletea baadhi ya mataji yanayoshindaniwa na yenye thamani kubwa sana timu ikiyashinda:

Kombe la Dunia la FIFA

Kinacholipa heshima kombe hili ni kwamba hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne, na baadaye huweza kulifanya kuwa na mvuto kutokana na muunganiko wa wachezaji kutoka ligi mbalimbali kuwa katika timu moja. Kombe hilo linakadiriwa kuwa na thamani ya $20M ambapo mshindi wa mwaka jana, Ufaransa aliondoka na $38M baada ya ushindi. Hilo ni kombe lenye thamani sana duniani.

Kombe la FA

Kombe hilo lina heshima kubwa ndani ya taifa la Uingereza ambapo klabu zinazocheza ndani ya taifa hilo huweza kushindana na kupata mshindi ambaye huondoka na kikombe hicho. Football Association Challenge Cup itampatia mshindi wake wa 2018/19 zawadi ya £3,600,000 pesa ambayo ina thamani kubwa. Na kwa sasa kombe hilo linashikiliwa na Chelsea.

Ngao ya Hisani ya Jamii ya FA

Hii huhusisha mshindi wa ligi kwa msimu huo na mshindi wa kombe la FA, ambapo wawili hao hukutana na mshindi atakayepatikana atapewa nafasi ya kuchukua heshima hiyo. Klabu za jiji la Manchester zinaongoza kwa kutwaa kombe hilo huku United wakilitwaa mara nyingi. Kiuhalisia huonekana ni kombe lisilo na umuhimu sana lakini huiongezea kipato klabu inayolichukua.

Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya

Linafahamika sana kwa jina la Kombe la UEFA. Klabu inayoshinda kombe hilo hupewa heshima ya pekee na kwa sasa rekodi inashikiliwa na Madrid ambao pia msimu uliopita walitwaa na kuwafanya kuwa na vikombe 13 hadi sasa. Mshindi wa 2018/19 atatunukiwa zawadi yenye thamani ya €19,000,000. Hiyo ni zawadi kubwa sana kwa hali ya kawaida.

Makombe mengine yenye heshima na yanayolipa sana ni Copa America, kombe la La Liga, Coppa Campioni D’Italia na lile la Ujerumani [Deutsche Meisterschale]. Pia, kuna tuzo ambazo huwa na thamani ya juu ambazo wachezaji huzipokea ambazo huwa na thamani sana zikiwemo Ballon d’Or, kiatu cha dhahabu kinachotolewa klabu bingwa Ulaya [European Golden Boot] na glovu za dhahabu zinazotolewa katika ligi ya Uingereza.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa