Kevin De Bruyne Anaamini kuwa Man City bado wana nafasi nzuri ya kumaliza vizuri msimu baada ya kupoteza taji la EPL.

City wanawatembelea Newcastle United Jumapili kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la FA, pia mwezi Agosti watakutana na Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa.

De Bruyne anaamini kuwa City hawatakwamishwa na kupoteza taji la EPL baada ya kurushusu kichapo kutoka kwa Chelsea kilichowazawadia ushindi wa mapema Liverpool ambao wamesota kwa miaka 30 kuinua taji lao.

Man City walishindwa kutetea ubingwa wao wa miaka miwili Alhamisi, lakini hii bado haijawafungia milango yote ya ubingwa klabu hii ambayo ilifanikiwa kuweka kibindoni mataji matatu msimu uliopita. Walishinda taji la tatu la Carabao Cup mwezi Machi, wana nafasi ya kushinda mataji mengine.

Wakifanya vyema kwenye robo fainali ya FA Cup wanasonga mbele na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji hilo.

Wakati huo, licha ya ushindani mkubwa uliopo katika Ligi ya Mabingwa, bado wanaweza kujitunzia heshima zaidi Ulaya ikiwa watashinda UCL. De Bruyne anaamini ni nafasi ambayo City bado wanayo na wanaweza kuitumia.

41 MAONI

  1. Man city timu nzuri sana na bado wananafasi ya kuwania makombe mengine kama uefa na fa sio mbaya bhana wapambane kwenye makombe mengine,

  2. Man city wapo vzr kikos kipana sema tuu msimu huu walipoteza baadhi ya mechi wakatoka kwenye mbio za ubingwa

  3. Man city bado wananafasi kubwa ya kushinda makombe mengine ingawa wanatakiwa kujilinda dhidi ya maadui wanaokutana nao uwanjani

  4. Mancity hawanabudi kujituma ili kuweza kuchukua FA lakini ikumbukwe kuna timu nyingine pia wanahitaji kuchukua FA.

  5. Man city wajipange kw a msimu ujao ila kwa msimu huu watamaliza kwenye nafasi hata ya pili au tatu maana lolote laweza tokea

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa