Waswahili husema, “lisemwalo lipo au linakuja”. Kupitia gazeti la The Sun, limeripoti kuwa Man City wanakwenda kumwaga pesa ili kumsajili Harry Kane.

Siku chache zilizopita, ilitangazwa kuwa Spurs wameikataa ofa ya kwanza ya City ya £100M ili kumsajili Kane. Pamoja na hayo, Daniel Levy alisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi na akiuzwa hatouzwa Uingereza, London kwa msisitizo mkubwa (akiwalenga Chelsea).

Mambo hubadilika, imeripotiwa kuwa Levy amebadilisha mawazo yake na kuamua kumpatia Kane kile anachokitaka (kuondoka Spurs), taarifa hii ya mabadiliko ya Levy amepatiwa wakala wa Kane ambaye pia ni ndugu yake – Charlie.

Man City, Man City Kumwaga Pesa Kwa Kane., Meridianbet
Gabriel Jesus kuwa chambo kukamilisha usajili wa Kane.

Hii ni taarifa kubwa na ya furaha kwa Kane kwani sasa anauona mwangaza wa kwenda Man City. Japokuwa, usajili wa kwenda Etihad hautokuja kirahisi. Man City watapaswa kutoa kitita cha £160M ili kumsajili Kane ambaye pia anaripotiwa kukubali mkataba wa mshahara wa £400,000 kwa wiki.

Kwa upande wa City, wapo tayari kutoa mchezaji mmoja kati ya Raheem Sterling, Riyad Mahrez, Gabriel Jesus na Bernado Silva kama sehemu ya usajili wa Kane kutoka Spurs. Endapo usajili huu utafanikiwa, Kane atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa pesa ndefu kwenye historia ya EPL. Rekodi hii kwa sasa inashikiliwa na Paul Pogba (Man United) aliposajiliwa kutoka Juventus kwa £89M.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa