Hakika mashetani wekundu wameamua kuwa mashetani kweli kwa wamiliki wa Man United. Mashabiki wa United kuendeleza maandamano mpaka pale wamiliki watakapoachia ngazi.

Baada ya kufanikiwa kuingia Old Trafford na kupelekea mchezo kuaghairishwa wikiendi hii, mashabiki wa United wametangaza kuendelea na maandamano. Safari hii, wanawalenga wadhamini wote wanaliowekeza ndani ya klabu hiyo.

Kupitia mtandao wa Twitter, kampeni rasmi ya #NotAPennyMore imeanza kusambaa miongoni mwa watumiaji wa mtandao huo. Hii ni hatua ya awali kuelekea maandamano makubwa zaidi yatakayoelekezwa kwa wadhamini wa Man United ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu zaidi na famili ya Glazers.

Mashabiki wa United wanaamini, endapo wadhamini hawa watasitisha mikataba yao ya kibiashara ambayo kwa sehemu kubwa inawafaidisha wanafamilia ya Glazers kuliko klabu, itakuwa ni nyongeza nzuri kwa kile wanachokitaka kwa Glazers kuachana na klabu hiyo.

Kupitia umoja wa mashabiki wa United, limetolewa tamko kwa wadhamini wote waliowekeza klabuni hapo kuchukua hatua stahiki kwani mashabiki wamedhamiria kuwaharibia soko lao kwa kila namna mpaka pale watakapo amua kuungana nao na kuijenga United upya bila uwepo wa Glazers kama wamiliki wa klabu hiyo.

Hakika Man United kumewaka moto, mashabiki wameamua kujitoa kwa kila wanachokiweza ili kuondoa utawala wa Glazers. Swali ni je, watafanikiwa?


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Man United, Man United: Kituo Kinachofuata, “Kwa Wadhamini”, Meridianbet

SOMA ZAIDI

18 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa