Baada ya maandamano ya mashabiki wa Man United katika dimba la Old Trafford jumapili hii, familia ya Glazers bado hawajatoa tamko lolote kuhusu tafrani iliyotokea.

Baadhi ya mashabiki wa The Red Devils waliovamia uwanja siku ya Jumapili na kupelekea mchezo wao dhidi ya Liverpool kughairishwa, walifanya hivyo kama sehemu ya kufikisha ujumbe wao kwa wamiliki wa klabu hiyo – familia ya Glazers.

Mashabiki wa United wanahitaji kuona wamiliki wa klabu hiyo wakiachia nafasi hiyo kwa kile wanachodai ni uendeshaji mbaya usio na faida kwa klabu tangu familia hiyo ichukue hatamu mwaka 2005.

Man United, Man United: Kwani Glazers Wanasemaje?, Meridianbet
Wanafamilia ya Glazers (Joel and Avram Glazers)

Licha ya purukushani zote za mashabiki wa United, familia ya Glazers haijasema chochote kuhusiana na maandamano hayo. Japokuwa, pengine Glazers watawajibu mashabiki wa Man United kwa kuwekeza zaidi kwenye dirisha la usajili linalofuata mwezi Julai mwaka huu.

Imeripotiwa kuwa, United wanajiandaa kuweka mezani dau la pauni milioni 90 kwa Spurs ili wamsajili nyota wao Harry Kane. Sambamba na Kane, United wanahusishwa na Jadon Sancho kwa mara nyingine mwaka huu. Hii ni baada ya dau la mchezaji huyo kushuka mpaka pauni milioni 85.

Je, endapo Glazers wataamua kufanya vitendo zaidi ya kuwajibu mashabiki kwa barua na mazungumzo ya wazi, watakuwa wamejisafisha na kustahili imani za mashabiki wa Man United?


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Man United, Man United: Kwani Glazers Wanasemaje?, Meridianbet

SOMA ZAIDI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa