Kama ilivyo kwenye NBA msimu huu. Kunako ulimwengu wa soka, Man United wamerudia kuandika historia iliyodumu kwa miaka 57 tangu 1964.

Man United walikuwa uwanjani jana usiku wakichuana na AS Roma kunako nusu fainali ya Ligi ya Europa. Matokeo ya 6-2, yaliwatosha vijana wa Ole Gunnar Solskjaer kuwaumiza Roma pale Old Trafford.

Hii sio mara ya kwanza kwa timu kufunga magoli 6 kwenye hatua ya nusu fainali kunako mashindano ya Ulaya. 1964, Real Madrid walifanya hivyo dhidi ya Zurich. Tangu 1964, hakuna timu iliyowahi kupata ushindi wa magoli hayo katika mchezo wowote wa nusu fainali ya mashindano ya Ulaya. United wamefanya hivyo baada ya miaka 57.

Man United, Man United Yarudia Historia ya 1964., Meridianbet
Cavani akishangilia goli dhidi ya AS Roma.

Bruno Fernandes, Edinson Cavani, Paul Pogba na Mason Greenwood walitosha kupeleka kilio kwa vijana wa Forenseca licha ya Roma kuongoza kwa matokeo ya 2-1 wakati wa mapumziko.

Kwingineko kwenye Ligi ya Europa, Arsenal wameshindwa kufua dafu dhidi ya Villareal ambayo inanolewa na aliyewahi kuwa kocha wa Arsenal – Unai Emery. Emery alitimuliwa Emirates na nafasi yake kuchukuliwa na Arteta ambaye aliambulia kipigo cha magoli 2-1.

Man United watarejea uwanjani Jumapili hii kukipiga dhidi ya Liverpool kwenye EPL kabla ya kuwafata AS Roma alhamisi wiki ijayo kwenye mchezo wa pili kwenye hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Europa.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa