Klabu ya Manchester City inaripotiwa kuwa inajiandaa kumpa Reuben Dias ofa ya mkataba wenye mkwanja mzuri zaidi baada ya kufanya vyema msimu wake wa kwanza Etihad Stadium.

Nyota huyu mwenye miaka 24 alisaini mkataba wa miaka sita alipowasili klabuni hapo akitokea klabuni Benfica msimu na amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 50 kwa msimu wa 2020-21.

Reuben Dias Manchester City

Kwa mujibu wa Dailystar, City wanatarajia kumpa Dias mkataba mpya ambao utamlipa takribani mara mbili ya mshahara wake anaolipwa kwa mkataba wa sasa wa £140,000 kwa wiki.

Mlinzi huyu alitajwa kuwa mchezaji wa msimu kwa msimu uliopita kwa EPL na pia alitwaa tuzo kama mchezaji bora wa FWA kwa kiwango chake bora cha msimu.

Manchester City wanajiandaa na msimu mpya, na Pep Guardiola anasaka kuwa na kikosi bora zaidi kwa kurekebisha baadhi ya maeneo ambayo yalionesha changamoto wanapoenda kutetea taji lao.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa