Kutoka jiji la Manchester, kocha wa timu ya Taifa ya Wales ambaye pia alikuwa mchezaji wa Man United, Ryan Giggs, amesomewa mashtaka dhidi yake na ameyakataa mashtaka hayo.

Giggs anashtakiwa kwa vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake wawili. Mmoja akiwa na umri wa miaka 30s na mwingine anamiaka 20s. Vitendo hivi vimetajwa kufanyika Novemba,2020 katika maeneo ya jiji la Salford.

Sambamba na mashtaka ya udhalilishaji, Giggs (miaka 47) pia amesomewa mashtaka ya kuwa na tabia ya ukorofi ambapo kesi hiyo inamuhusisha na vitendo hivyo vilivyofanyika kati ya mwezi Disemba 2017 na Novemba 2020.

Manchester, Manchester: Ryan Giggs Akataa Mashtaka., Meridianbet
Ryan Giggs akiwa mazoezini na kikosi cha Wales

Giggs ambaye pia ni miongoni mwa wamiliki wa timu ya Salford City FC, alihudhuria mahakama ya Manchester ambapo alithibitisha anuani yake pamoja na tarehe yake ya kuzaliwa kabla ya kusomewa mashtaka dhidi yake.

Licha ya kusikiliza mashtaka aliyosomewa, Giggs ameyakataa mashtaka yote na mahakama imempatia dhamana ikiwa ni sambamba na masharti ya kutokuwa karibu na wanawake wote anaohusishwa nao kwenye mashtaka yake.

Keshi ya Giggs itasikilizwa tena Mei 26 katika mahakama ya Manchester. Kutokana na muendelezo wa kesi hii, Giggs ataendelea kuwa nje ya uwanja wakati huu ambapo timu ya Taifa ya Wales inajiandaa na mashindano ya Euro ikiwa chini ya kocha msaidizi.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa