Timu ya Manchester City imetangaza kuwa imepata hasara ya Euro Millioni 126 msimu uliopita kutokana na Korona. Kiasi hicho cha fedha kinamaanisha City imepata punguzo la 11% ya mapato yao msimu uliopita!

Katika taarifa rasmi kutoka kwa Machester City mapato mengi ya Klabu hiyo hayakuhusisha baadhi ya fedha kama vile mauzo Leroy Sane kwenda Bayern kwa sababu malipo yalichelewa. Taarifa rasmi inadai kuwa kitendo cha ligi hiyo kusimama kati ya machi na juni mwaka jana kulichangia kwa kiwango kikubwa kupungua kwa mapato.

Licha ya mapato hiyo Manchester City bado wanaimani kubwa na kupata mapato makubwa msimu huu kwa kuwa wamekuwa na jitihada nyingi za mapato.

Taarifa hiyo ya mapato itawafanya Manchester City kuangalia upya kiwango cha fedha kwa ajili ya usajili. Kulikuwa na tetesi juu ya kutaka huduma ya Haaland na Grealish je itawezekana?

Timu hiyo kongwe wanaongoza Premier League wakiwa na alama 74, huku wakiwaacha maasimu wao Man United kwa alama 14. Njia ya kuchukua ubingwa msimu huu ipo wazi na wanaweza kupata fedha nyingi humo, ambao walishinda mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA dhidi ya Dortmund jana usiku. Magoli yao yalifungwa na Kelvin De Bruyne na Phil Foden dakika za mwishoni kabisa.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa