Kipa namba moja wa Simba sc na Taifa Stars, Aishi Manula amefunguka siri ya kiwango chake bora anachokionesha msimu huu 2020/2021.

Katika mahojiano na Ahmed Ally, mtangazaji wa Azam Tv baada ya mechi kati ya Simba na Kagera Sugar ambapo Simba walishinda 2-0, Manula alieleza namna ambavyo ukuta wake wa mabeki unavyomfanya awe katika kiwango kizuri.

Manula amesema ushirikiano anaopata kutoka kwa Joash Onyango, Pascal Wawa, Mohammed Hussein na Shomari Kapombe ni mkubwa na ndiyo unaomfanya kuzidi kung’ara siku hadi siku.

Manula ameongeza kuwa wakati mwingine anawaelekeza walinzi wake kwa lugha kali (kuwafokea) ili kutimiza malengo ya kuhakikisha timu inafanya vizuri.

“Kiwango changu kinatokana na ushirikiano baina ya safu yetu ya ulinzi. Mabeki wamekuwa wakihakikisha sifikiwi kirahisi na ikitokea wamepitwa na mimi nasahihisha makosa yao,” alisema Manula.

Manula

Manula amesema kwa sasa malengo yake ni kuhakikisha anaisaidia timu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, kufikia malengo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Mlinda mlango huyo amecheza mechi 13 bila kuruhusu bao (clean sheet) akiwa anaongoza miongoni mwa makipa wote wanaoshiriki Ligi Kuu.

Aishi alieleza kutamani kucheza nje za nchi lakini mpaka sasa hajapata ofa yoyote kutoka kokote, japo ya tetesi za Mamelodi Sundowns pamoja na Al Merekh kuhitaji huduma yake, akiwa mkataba wa mwaka mmoja na Simba na endapo timu yoyote itahitaji kumsajili italazimika kuvunja mkataba kwa kununua mwaka huo mmoja.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Manula, Manula: Mabeki Wanasaidia Kukuza Ubora Wangu, Meridianbet

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa