Kocha wa zamani wa Birmingham Marc Skinner ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Manchester United kwa upande wa wanawake.

Skinner alitangaza kujiuzulu wadhfa wake huko Orlando Pride wiki iliyopita, na kumaliza uvumi kuwa alikuwa ni mbadala wa Casey Stoney.

Alhamisi United wamethibitisha uteuzi wake. Marc Skinner ambaye ana miaka 38 amesaini mkataba wa miaka miwili na United.

Marc Skinner Kocha Mkuu Man United
Marc SkrinnerKocha huyu alianza kazi yake kama kocha miaka nane iliyopita huko Birmingham, akipitia ngazi kadhaa na kufika Orlando Pride mwaka 2019.

Marc amesema kuwa anafurahi kuwa United na ni mpango wake kuhakikisha anashirikiana na uongozi kupata mafanikio makubwa klabuni hapo.

Makamu Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward amesema kuwa wanamtambua Skinner kama mmoja wa makocha wenye uzoefu, ni furaha yao kumuona anarejea EPL baada ya kutumia mda fulani kwenye soka la Marekani.


KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa