Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amedokeza kwamba Marcus Rashford anaweza kurejea dimbani baada ya kufanyiwa operesheni.

Staa huyu anatarajiwa kurejea kwenye mechi ya Ligi Kuu na Leicester City mnamo Oktoba 16.

Mshambuliaji huyo alifanyiwa upasuaji wa bega wakati wa msimu wa joto na bado hajahusika na mechi yoyote ya Mashetani Wekundu kwa msimu huu 2021-22.

Hivi karibuni Marcus Rashford amepigwa picha kwenye mazoezi, na kulikuwa na madai kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza angeweza kuwepo dimbani kabla ya mapumziko ya kimataifa.

Marcus Rashford
Marcus Rashford alifanyiwa upasuaji wa bega na yupo tayari kurejea.

Hata hivyo, Solskjaer aliambia tovuti rasmi ya Man United kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kurejea baada ya seti nyingine ya mechi za kimataifa mnamo Oktoba.

Mashetani Wekundu wana mechi tatu za nyumbani dhidi ya Aston Villa, Villarreal na Everton kabla ya kusafiri Oktoba 16 kwenda King Power kumenyana na Leicester.

Rashford, ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa nchi yake kwenye Euro 2020 licha ya shida zake za majeruhi, alifunga mabao 21 na kutoa asisti 15 kwenye mechi 57 za Man United kwa msimu uliopita.


FUNGA BAHATI YAKO NA MERIDIANBET.

Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa