Mchezaji watimu ya taifa ya Austria, Marko Arnautovic ameondolewa kwenye majina ya wachezaji wataoendelea kushiriki michuano ya Euro 2020 na UEFA baada ya utovu wa nidhamu alioonesha kwa mchezaji wa North Macedonia.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu za Stoke City na West Ham za Uingereza, sasa anacheza katika klabu ya Shangai Port ya China alitulizwa na mchezaji mwenzake David Alaba mnamo dakika ya 89.

Marko Arnautovic ambaye ana asili ya Serbia alionekana kutoa maneno ya kashfa kwa mchezaji wa timu pinzani Egzon Bejtulai.

Baada ya mchezo na ripoti hiyo kutoka, Marko Arnautovic alitoa ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza kuwa yeye sio mbaguzi wa rangi ila kilichotokea kwenye mchezo huo ni hasira tu za mchezo.

Taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji wa mashindano ziliandika kuwa “Tunamfungia mchezaji wa timu ya taifa ya Austria, Marko Arnautovic mchezo mmoja unaofuata ambao angeweza kucheza kwa kosa la kumtusi mchezi mwingine”.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa