Mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA kati ya Leicester na Southampton tarehe 18 baadae mwezi huu unatazamiwa kuwa kama jaribio la kuangalia uwezekano wa mashabiki kurudi uwanjani.

Nusu fainali hiyo itachezwa katika uwanja wa Wembley ambapo wataruhusiwa tu wakazi 4000 wa eneo linalozunguka uwanja huu kushuhudia mechi hiyo.

Kumekuwa na vizuizi vinavyozuia mikusanyiko mikubwa ya watu katika shughuli mbalimbali za kimichezo nchini Uingereza toka mwezi Disemba.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson mapema mwezi uliopita alielezea namna ambavyo serikali yake inategemea kulegeza vizuizi nchini kote.

Inatumainiwa kwamba Mchezo wa fainali wa Euro 2020 utakuwa na watu wengi zaidi.

Timu nyingi duniani zimekuwa zikilalamika kufanya vibaya kutokana na ukosefu wa mashabiki uwanjani. Katika mahujiano ya hivi karibuni, mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah alisema anahisi timu yake inafanya vibaya kutokana na kuzoea kuwaona mashabiki zao.

Korona imesababisha shughuli mbalimbali za kimichezo zikisitishwa kutokana na kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Je huu unaweza kuwa ni wakati sahihi kwa mashabiki kurudi uwanjani?

UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

mashabiki, Mashabiki Kurudi Uwanjani Nusu Fainali Kombe la FA, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa